Mwinyi azindua mbio za mwenge 2026

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi, amezindua Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026 na kuwataka Watanzania kuendelea kulinda amani, kudumisha umoja na kuimarisha uzalendo kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Akizungumza leo Aprili 2, 2026 katika Uwanja wa Gombani, Pemba, Rais Mwinyi amesema  kuwa amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa ni msingi muhimu wa maendeleo endelevu, akisisitiza umuhimu wa kuulinda na kuudumisha Muungano wa Tanzania.

Aidha amebainisha kuwa taasisi zote na wananchi kwa ujumla wanapaswa kuheshimu utu, haki, usawa na utawala wa sheria ili kuimarisha mshikamano wa Taifa. Amesema Mwenge wa Uhuru unaendelea kuwa chombo muhimu cha kuhamasisha uzalendo, uwajibikaji na mapambano dhidi ya changamoto za maendeleo zikiwemo umasikini, ujinga na maradhi.

Rais Mwinyi pia amewahimiza Watanzania kupinga ubaguzi wa aina yoyote na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana na rushwa, dawa za kulevya pamoja na magonjwa kama UKIMWI na malaria.SOMA: Kiongozi mbio za mwenge ataka kasi ukusanyaji mapato

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha huduma za afya, kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya na kupunguza maambukizi ya malaria, huku akisisitiza ushirikiano wa wadau wote katika kufanikisha maendeleo ya Taifa. Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeanza katika Mkoa wa Kusini Pemba na zinatarajiwa kufikia kilele chake Oktoba 14, 2026 mkoani Rukwa, zikiwa na kaulimbiu: “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane.”

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Mình biết đến CM88 qua bạn bè giới thiệu và thử truy cập tại https://87sasprosnowmeprona.sa.com/
    thì thấy trải nghiệm khá ổn. Giao diện thiết kế đơn giản, dễ hiểu nên người mới cũng dễ làm quen. Mình chơi thử casino live và thấy khá mượt, hình ảnh rõ nét, không bị giật lag. Theo nhiều đánh giá thì CM88 có hệ thống vận hành ổn định và đa dạng game nên phù hợp nhiều người chơi khác nhau . Tuy nhiên, anh em vẫn nên chơi với mức vốn hợp lý để tránh rủi ro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button