SMZ kuimarisha viwanja vya michezo

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inalenga kuviimarisha viwanja vya michezo nchini ili viwe bora na kukidhi viwango vya kimataifa.
“Serikali itaendelea ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inalenga kuviimarisha viwanja vya michezo nchini ili viwe bora na kukidhi viwango vya kimataifa.
Akizungumza Oktoba 1, 2025 katika fainali ya michuano ya Yamle Yamle kati ya Mazombi FC na Muembe Makumbi Combine kwenye Uwanja wa New Amani Complex, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dk. Mwinyi alisema Serikali imewekeza fedha nyingi kujenga viwanja vya kisasa vitakavyowawezesha vijana kushiriki michezo na kukuza vipaji vyao. “Serikali itaendelea kujenga viwanja vya kisasa katika kila wilaya ili michezo iwe sehemu ya ajira na maendeleo ya vijana,” alisema Dkt. Mwinyi.

Aidha, aliipongeza Zanzibar Broadcasting Corporation (ZBC) kwa kuendeleza michuano hiyo kwa msimu wa saba mfululizo na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa udhamini wake kama mdhamini mkuu.
Katika mchezo huo wa fainali uliokuwa na ushindani mkubwa, Muembe Makumbi Combine iliibuka bingwa baada ya kuifunga Mazombi FC mabao 3–0, yote yakipatikana katika kipindi cha pili.

Mara baada ya mchezo, Rais Dkt. Mwinyi aliikabidhi Muembe Makumbi Combine kitita cha Sh milioni 20 pamoja na kombe la ubingwa wa msimu wa 2025/26, huku Mazombi FC ikipokea Sh milioni 10.
Michuano hiyo ya Yamle Yamle ilibeba kaulimbiu: “Amani Amana.”kujenga viwanja vya kisasa katika kila wilaya ili michezo iwe sehemu ya ajira na maendeleo ya vijana,” alisema Dkt. Mwinyi.
Aidha, aliipongeza Zanzibar Broadcasting Corporation (ZBC) kwa kuendeleza michuano hiyo kwa msimu wa saba mfululizo na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa udhamini wake kama mdhamini mkuu.
Katika mchezo huo wa fainali uliokuwa na ushindani mkubwa, Muembe Makumbi Combine iliibuka bingwa baada ya kuifunga Mazombi FC mabao 3–0, yote yakipatikana katika kipindi cha pili.
Mara baada ya mchezo, Rais Dkt. Mwinyi aliikabidhi Muembe Makumbi Combine kitita cha Sh milioni 20 pamoja na kombe la ubingwa wa msimu wa 2025/26, huku Mazombi FC ikipokea Sh milioni 10.
Michuano hiyo ya Yamle Yamle ilibeba kaulimbiu: “Amani Amana.” SOMA: Uwanja wa kisasa wakamilika Zanzibar