Umoja Ni Nguzo ya Amani

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza umuhimu wa kulinda amani, umoja na mshikamano nchini, akihimiza wananchi kuondoa ubaguzi na kuimarisha upendo katika jamii.

Amesema umoja wa wananchi ni msingi wa utulivu wa taifa, na kila mmoja ana wajibu wa kulinda tunu hizo kwa vitendo. Kauli hiyo ameitoa Aprili 3, 2026, baada ya kushiriki Sala ya Ijumaa iliyoambatana na dua maalum katika Msikiti wa Mzee Ali Hassan Mwinyi uliopo Mangapwani, Unguja.

Amewataka  waumini kuepuka makundi ya chuki na migawanyiko, akisisitiza kuwa dini inahimiza amani na uvumilivu. Dua hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Mke wa Rais, Mama Mariam Mwinyi, pamoja na viongozi wa dini na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Pia walizuru kaburi la hayati Ali Hassan Mwinyi kwa ajili ya kumuombea dua.SOMA: Dk Mpango: Tulinde amani kumuenzi Nyerere

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button