RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar bado ina fursa nyingi za uwekezaji katika Sekta mbalimbali na kuwakaribisha wawekezaji kutoka Saudi Arabia kuwekeza nchini.
Ameyasema hayo alipozungumza na wawekezaji na wafanyabiashara wa Saudi Arabia waliofika Ikulu kuonana naye wakiwa katika ziara maalum Tanzania ya kubaini maeneo ya Ushirikiano, Uwekezaji na Biashara.

Dk Mwinyi amezitaja sekta nyingine ambazo zina fursa za wwekezaji kuwa ni kilimo, mafuta, gesi na miundombinu na kuushukuru ujumbe huo kwa kuamua kuja Zanzibar kwani ziara hiyo itafungua ukurasa mpya wa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na akiwasisitiza kuwa mabalozi wazuri wa kuzitangaza fursa za Zanzibar nchini kwao.

Naye Rais wa Shirikisho la Jumuiya za Wafanyabiashara wa Saudi Arabia Hassan, Alhuwayz amesema wana nia ya dhati ya kuimarisha ushirikiano na Zanzibar hususani katika masuala ya biashara na uwekezaji kwani tayari wamebaini kuwepo kwa fursa nyingi pamoja na kuvutiwa na maendeleo yaliyofikiwa na Zanzibar na hali ya Amani iliopo.

Wakati huo huo Rais Dk Mwinyi ameshuhudia utiaji saini wa mikataba baina ya Zanzibar na Saudi Arabia ikiwemo ya ushauri kati ya Zanzibar na Kampuni ya Saudi Arabia African Investment and Development Company na Mkataba wa ushirikiano baina ya Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara wa Zanzibar (ZNCC) na Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara wa Saudi Arabia kwa lengo la kuimarisha uwekezaji wa kimkakati na kukuza uchumi wa Zanzibar.
Hi there Dear, are you truly visiting this site on a
regular basis, if so afterward you will definitely obtain pleasant know-how.