Mzee Karume aliruhusu Wazanzibar, Waarabu kuoana

Zanzibar

MAPINDUZI ya Zanzibar yamefikisha miaka 61.  Kama ungekuwa umri wa mtu bila shaka angekuwa na watoto, wajukuu na pengine hata vitukuu kadhaa.

Lengo kuu la mapinduzi hayo lilikuwa kubadili maisha ya Wazanzibari kutoka kudharauliwa, kubaguliwa na kunyanyaswa na hatimaye kuwa na maisha yanayojali utu, heshima, usawa na haki za binadamu pamoja na maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Hata baada ya Uhuru wa Zanzibar mwaka 1963, serikali iliyorithi madaraka ilikuwa ya wachache hali ili youacha umma wa Wazanzibari kuendelea kuishi katika maisha magumu na mateso ndani ya taifa lao huru.

Advertisement

Hapo ndipo ulipokuja umuhimu wa mapinduzi ili kuondoa serikali ya kidhalimu inayohudumia wachache; serikali onevu, yenye ubaguzi na yenye mateso lukuki kwa wananchi iliyowaacha Wazanzibari wengi katika lundo la umasikini huku wakidanganywa kuwa wako huru.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya kihistoria, Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12,1964 yalilenga pia kujenga ustawi wa wanan chi wote na kuwawezesha kufaidi matunda ya uhuru wao yakilenga pia kuwapa wananchi wote fursa sawa za elimu.

Hii ni kwa kuwa elimu katika serikali ya kikoloni ilitolewa kwa kuzingatia ubaguzi mkubwa ukiwamo wa rangi kwa kuwapen delea Waarabu na familia zilizounga mkono wakoloni na kuwabagua wananchi wengi.

Ndio maana baada ya mapinduzi hayo matukufu, wananchi wa Zanzibar walipata fursa sawa ya elimu na huduma nyingine walizostahili kutoka katika serikali yao.

Huduma za afya ni eneo lingine ambalo wananchi wa Zanzibar walikuwa wakibaguliwa na kuonewa hadi Mapinduzi ya Zanzibar yalipowakomboa.

Baada ya Mapinduzi hayo Serikali ya Zanzibar chini ya , Sheikh Abeid Amani Karume ikaanza kutekeleza shabaha ya kuinua hadhi na hali ya wananchi na kuwa fanya waachane na unyonge waliokuwa nao kutokana na madhila ya utawala wa kikoloni chini ya sultani.

Katika kutekeleza hilo, Rais Karume alitumia mbinu mbalimbali kuwafanya wananchi wajisikie na kujitambua kuwa wao ni sehemu ya Wazanzibar na kwamba, waliokuwa na haki ya kufaidi rasilimali za taifa lao ambazo kutokana na misingi iliyojengwa na wakoloni zilikuwa zikiwanufaisha wakoloni.

Moja ya misingi iliyowe kwa na wakoloni kuhakiki sha kuwa jamii ya Waarabu inakuwa na hadhi kubwa huku Waswahili wakikan damizwa na kuwa katika hali ya chini ni ubaguzi uliowapendelea zaidi watu wenye asili ya Kiarabu dhidi ya Waswahili (Wazanzibar).

Mzee Karume

Inaelezwa na vyanzo mbalimbali kuwa, ili kuzuia kabisa Waswahili wasipate hadhi na pengine hata kuwafikia Waarabu, serikali ya kikoloni ilipiga marufuku Waswahili kuoa au kuolewa na Waarabu. Hii ni kwa kuwa Waza zibar kama Waswahili, walichukuliwa kama watumwa na ilikuwa fedheha na aibu kubwa kwa Mwarabu kuolewa au kuoa Mswahili.

Mwanasiasa mkongwe, Mzee Paul Kimiti aliyekuwepo wakati wa Mapinduzi ya Zanzibar, ananukuliwa akisema kutokana na misingi hatari ya ubaguzi iliyoachwa na wakoloni baada ya mapinduzi, Rais Karume aliamua kuruhusu Waswahili kuoa au kuolewa na Waarabu.

Karume aliruhusu ndoa hizo ili kuvunja kuta za kibaguzi ziliowekwa na wa koloni dhidi ya Wazanzibar.

Aidha, alilenga Waswahili waliodharauliwa na kubaguliwa kutokana na rangi ya ngozi zao wa rudishe hadhi yao dhidi ya unyonge kutokana na kukata tamaa kulikotokana na kudharauliwa.

Katika vyanzo mbalimbali, Kimiti anasema baada ya ruhusa ya kuoana kati ya Waswahili na Waarabu, heshima kwa Wanzanzibar ilianza kurejea kwa kuwa walianza kuzaliwa watoto wenye rangi mchanganyiko hali iliyoweka ugumu kwa ubaguzi kuendelea.

“Wakaanza kuzaliwa watoto chotara ambao waliua kabisa ule ufalme wa Waarabu kwa kuwa watawezaje kuwadharau Waswahili wakati wameungana na kuunda familia moja na kuchanganya damu za Waswahili na Waarabu, “ anasema.

Waswahili walianza kujiamini na kujiona ni kitu kimoja na kwamba ni sehemu ya Wazanzibari wenye haki sawasawa na wengine ambao awali walionekana bora kuliko wengine.

Baada ya kufaulu kuwaleta pamoja Wazanzibari, Karume alianzisha Umoja wa Vijana wa kujitolea kulinda mapinduzi dhidi ya wanyang’anyi ambao ha wakupenda kuona Wazanzibar wanakuwa na thamani mbele ya jamii.

Mzee Kimiti ambaye ni Mtaalamu wa Kilimo na aliyewahi kuwa Waziri wa Kilimo katika Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere anasema mwaka 1971, Karume aliitisha mkutano Chake Chake Kisiwani Pemba ili kujenga uwezo wa vijana kupamba nia taifa lao.

Mapinduzi ya Zanzibar yanasemwa kuwa kiini cha kuwaunganisha Watanganyika na Wazanzibari kuwa watu wamoja na kuzung umza lugha moja kwa kuwa yalitoa nafasi kwa viongozi wa mataifa yote kufanya mipango ya kuwaunganisha kupitia Muungano.

“Mapinduzi ya Zanzibar yaliimarisha ulinzi na usala ma kwa Tanzania nzima kwa kuwa baada ya mapinduzi, serikali ya kizalendo ilikuwa na mashaka makubwa kuto kana na maadui kutoka nje ambao hawakufurahishwa na mapinduzi hayo,” anasema Mzee Kimiti.

Juhudi za kuinua maisha ya wanyonge zilianza wakati wa Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Sheikh Abeid Amani Karume kwani baada ya mapinduzi hayo, kiongozi huyo aliimarisha makazi ya wananchi wa Visiwa vya Unguja na Pemba kwa kuwajengea majengo makubwa ya ghorofa ili kuwakwamua dhidi ya hali duni ya maisha.

Katika uongozi wa Karume, serikali ilijitahidi kujenga barabara, viwanja vya ndege, viwanda na kui marisha kilimo hasa kilimo cha zao la karafuu lililoipatia Zanzibar umaarufu mkubwa kiasi cha kuitwa Visiwa vya Harufu ya Karafuu. Serikali zote zilizofuata ziliendeleza kile kilicho anzishwa na waasisi wa mapinduzi.

Ndio maana hata Serikali ya Awamu ya Nane inay oongozwa na Rais Hussein Mwinyi imeamua kuendelea kutafsiri kivitendo dhana ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kujenga miradi mbalim bali mipya kuimarisha na kujenga zaidi maisha ya wananchi.

Sekta ya viwanda ndio iliyopewa kipaumbele zaidi kutokana na sera ya uchumi wa viwanda itakayorahisisha utengene zaji wa nafasi nyingi za ajira kwa wananchi hali itakayowawezesha kukidhi mahitaji mbalimbali na kujenga taifa.

Chini ya Dk Mwinyi, Serikali imejitahidi pia ku jenga ustawi wa Wazanzi bari kwa kuimarisha sekta ya uchumi kupitia ubunifu wa dhana ya uchumi wa buluu. Dhana hii inagusa uchu mi wa mazao ya bahari kama samaki na pia, sekta za gesi na mafuta pamoja na utalii na kilimo hasa cha mwani na mazao mengine yanayotokana na bahari.

Kimsingi, Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika usiku Januari 12, 1964 kwa Wazazibar kutwaa Kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello. Okello aliyekuwa akiishi Pemba, alitokea Uganda miaka michache kabla ya kufanyika kwa mapinduzi hayo.

Ndani ya Zanzibar, Okello alipata umaarufu kuwa ni kijana shupavu na ni miongoni mwa makuli na wabeba mizigo wa meli zilizoingia na kutoka ban darini Zanzibar.

Wakati huo kulikuwa na fukuto lililoashiria macha fuko ya kisiasa yaliyokuwa yakiongezeka ndani ya Unguja na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa kilichotokea mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu miaka 50, tangu mwaka 1911 na kurithisha madaraka kwa mwanawe, Sultani Jamshid aliyekuwa sultani wa mwisho visiwani Zanzibar.