Dira 2050 yalenga kasi ya maendeleo

WAZIRI Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba amesema Dira Mpya ya Taifa ya Maendeleo inatarajiwa kuanza kutumika hadi mwaka 2050, huku akiwahimiza wadau kuandaa vipindi vitakavyoelezea historia na hatua za maendeleo zilizofikiwa na Serikali ya Tanzania.

Dk. Nchemba ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 110 wa Wadau wa Elimu kwa Umma. Amesema ni muhimu kuangazia mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 25 ya utekelezaji wa dira ya awali hususan katika sekta za mawasiliano, miundombinu, afya na huduma za kijamii.

Hapo awali huduma za mawasiliano zilikuwa na changamoto kubwa lakini kupitia utekelezaji wa mipango ya maendeleo hali imeimarika kwa kiasi kikubwa. Ameongeza kuwa dira mpya inalenga kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. SOMA: Samia: Ilani ya CCM imezingatia maudhui Dira ya maendeleo 2050

Amesema vijana wa sasa hawawezi kufahamu baadhi ya mifumo ya zamani kama matumizi ya stempu au masanduku ya posta, jambo linaloonyesha mabadiliko makubwa ya kiteknolojia. Hivyo, amesisitiza umuhimu wa wadau na wachambuzi wa masuala ya umma kuwaelimisha wananchi kuhusu historia ya maendeleo ya taifa.

“ Baada ya uhuru kulikuwa na shule tano tu za ufundi, zikiwemo Ifunda, Tanga na Moshi, lakini kwa sasa zimeongezeka hadi kufikia 103, hatua inayowawezesha vijana wengi kupata elimu ya ufundi na stadi za kazi”, alimalizia.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. the potential with this is endless…,

    This is what I do….. http://www.giftpay7.vip

  2. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

  3. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button