Nabi kicheko mashabiki bure kesho

KITENDO cha klabu ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini kutangaza mashabiki waingie bure kwenye mechi ya marudiano Kombe la Shirikisho Afrika, hakijamshtua kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi na badala yake anaona freshi tu.

Nabi amezungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa nchini humo, ambapo ameeleza kuwa klabu yake pia inapenda kucheza mbele ya mashabiki wengi kwa kuzingatia uzoefu wa wachezaji wake.

“Nina wachezaji wenye uzoefu wa kutosha wa kucheza mechi za namna hii,” amesema Nabi.

“Tumesahau kuhusu faida ya ushindi wa 2-0 tulioupata kwenye uwanja wa nyumbani. Huu ni mchezo mwingine na tuko na mpango mwingine wa dakika 90 za hapa.” ameongeza Nasreddine Nabi.

1 comments

Comments are closed.