Naibu Waziri awapa somo wataalamu wa uthamini

MOROGORO: NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Kaspar Mmuya amewataka wataalamu wa uthamini nchini kufanya kazi kwa uadilifu, weledi, kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya taaluma zao ili kuepuka kufanya kazi kwa kusukumwa na maslahi binafsi.

Mmuya amesema hayo kwa niaba ya Waziri wa Ardhi wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Leonard Akwilapo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa sita wa Mwaka Bodi ya Usajili ya Wathamini (VRB) uliofanyika mkoani Morogoro.

Amesema ili kufikia malengo hayo, wizara inapaswa kuandaa na kutekeleza mpango wa mafunzo endelevu ya matumizi ya teknolojia na mabadiliko yake ya mara kwa mara.

Naibu Waziri amesema hatua hiyo ni katika kazi za kila siku ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia katika kutekeleza majukumu yao na kuwahudumia wananchi kwa wakati katika sekta ya ardhi.

Mmuya amewataka wathamini kutenda haki wanapotekeleza majukumu yao ikiwa ni kutafsiri kwa vitendo dhamira ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ya kufanya kazi kwa kuzingatia utu.

“Ni wajibu  tutende haki kwa watu wetu tunaowasimamia na kama hufanyi vema kwa wale unaowasimamia thamani yako wewe kwao iko wapi? “ amehoji.

“ …Wathamini wote mnapofanya kazi zenu zingatieni thamani halisi ya mali inayothaminiwa tofauti na hivyo kupoteza uhalali wa kazi zenu, imani ya wadau wenu, mapato ya serikali pia kuwanyima haki wale wanaostahili kupata haki stahiki kwa mali zao,” amesisitiza Mmuya.

Pia amewaagiza watendaji wa wizara hiyo, kuwa wizara ishirikiane na wathamini wa sekta binafsi kufanya kazi za uthamini na kutumia fursa ya uwepo wa wathamini binafsi katika kutoa huduma kwa kuzingatia Serikali inayoongozwa na Rais Dk  Samia inasisitiza zaidi ushirikiano na sekta binafsi kwa maendeleo ya Taifa.

Naibu Waziri pia amewataka Wathamini wanapotekeleza majukumu yao kulinda mazingira na rasilimali za asili kwa kuzingatia athari za kimazingira, ufanisi wa nishati, maendelezo ya kijani na ustahimilivu wa mabadiliko ya tabia nchi.

Mmuya amehimiza  matumizi ya mbinu endelevu, na kuhakikisha thamani ya ardhi na mali inajumuisha pia urithi wa asili kwa maendeleo ya Taifa.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Wathamini ,Zidikheri  Mudeme ameishukuru  Serikali kwa kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Wathamini wote wa Serikali na sekta binafsi .

Amesema wanaowajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa maslahi ya taifa na kuwahudumia watanzania kwenye sekta ya Uthamini na kuongeza kuwa mikutano hiyo imekua nyenzo nzuri ya kujadili mambo mbalimbali yanayowakabili katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo, Lucy Kabyemera katika hotuba yake ya kumkaribisha Naibu Waziri kufungua mkutano huo, amesema  Wathamini wamepokea vizuri Mfumo wa e-Ardhi na wanautumia na  ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dk Samia ya kuwahudumia wananchi kupitia mifumo ili kurahisisha utoaji wa huduma za ardhi kote nchinio.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
    .
    Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button