WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Arusha, wamemchagua Namelok Sokoine kuwa mwakilishi wa mkoa huo katika nafasi ya NEC Mkoa kuwakilisha chama hicho taifa.
Akitangaza matokeo hayo leo Aprili 5, 2023, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda alimtangza Nameloj Sokoine kwa kupata kura 39 na kumwangusha mpinzani wake wa karibu mfanyabiashara, Hussein Gonga aliyeambulia kura 16.
Pinda wajumbe waliopiga kura walikuwa 67 na nafasi ya tatu ilishikwa na Daniel Palangyo alikuwa akitetea nafasi ya NEC kwa kupata kura 5, nafasi ya nne ni Judith Mollel aliyepata kura 3, Elibahati Lowassa na David Lemilla waliopata kura 2 na wagombea wengine Novatus Makunga, Prof. Samweli Ilila na Abdullazi Mawia hawakupata kura.
Pinda ambaye alikuwa mfanyakazi mlezi wa CCM Mkoa Arusha, aliwataka wajumbe kumpa ushirikiano Namelok katika kuifanya kazi yake vizuri na kuacha kumvua shati, kwani hiyo sio stahili ya uongozi ndani ya chama.
Namelok amewataka wana CCM kuvunja makundi kwani CCM ni moja na kundi lililobaki ni moja la Chama Cha Mapinduzi na sio vinginevyo.
Gonga aliwashukuru viongozi wa chama kwa jinsi walivyoendesha uchaguzi wa wazi na huru na yote aliyotaka kuyafanyia kazi iwapo angeshinda sasa atayapeleka kwa Namelok na atashirikiana naye kwa hali na mali.