Nanauka ashinda kura za maoni Mtwara Mjini

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mtwara Mjini kimetangaza matokeo ya kura za maoni nafasi ya ubunge jimbo la Mtwara mjini kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Akitangaza matokeo hayo leo Agosti 5 mwaka huu, Katibu wa CCM Walaya ya Mtwara Mjini Fadhili Mrami amesema kura halali ni 5,303 zilizopigwa ni 4,564 na kura zilizoharibika ni 739.

Aidha jumla ya wagombea wa nafasi hiyo ni sita hivyo amemtangaza Joel Nanauka kati ya wagombea hao kuwa mshindi katika matokeo hayo kwa kupata kura 2045 akifuatiwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mtwara mjini Hassan Mtenga aliyepata kura 1610.

Wagombea wengine ni Judith Nguli aliyepata kura 582, Baisa Baisa kura 146, Zhia Adinani kura 95 pamoja na Engeltraud Mbemba aliyepata kura 46.
Aidha matokeo hayo ni katika kata 18 za Jimbo la Mtwara mjini.

