Napoli yaitaka saini ya Lukaku kwa mkopo

TETESI za usajili zinasema klabu ya Napoli imewasilisha ofa kumsajili Romelu Lukaku kwa mkopo huku kukiwa na chaguo la kumnunua kwa pauni milioni 25.5.

Lukaku, aliyejiunga na Chelsea mwaka 2021 kwa ada ya pauni milioni 98 aliachwa katika kikosi cha kocha Enzo Maresca kilichopokea kichapo cha mabao 2-0 toka kwa Manchester City Agosti 17 katika mchezo wa ufunguzi Ligi Kuu England na hajacheza The Blues kwa zaidi ya miaka miwili.

SOMA: Villa yamuelewa Lukaku, yeye akataa

Ametumikia misimu miwili iliyopita kwa mkopo katika klabu za Inter Milan na Roma, mtawalia, na sasa anaweza kurudi tena Italia kuchezea klabu ya tatu tofauti.

Chelsea inasisitiza kwamba inataka kumuuza Lukaku kwa ada inayokaribia kipengele cha kumwachia cha pauni milioni 36 huku fowadi huyo akiwa bado ana miaka miwili imebaki katika mkataba wake Stamford Bridge.

Habari Zifananazo

Back to top button