TETESI za usajili zinasesema Aston Villa imekubaliana dili na Chelsea kumsajili mshambuliaji Romelu Lukaku, ambaye kwa sasa anakataa kuingia katika mazumgumzo na klabu hiyo ya kocha Unai Emery. (Il Mattino – Italy)
Lukaku anakusudia kuungana na Antonio Conte katika klabu ya Napoli na amekubali punguzo la mshahara kulazimisha kuondoka Chelsea. (Chronicle NG)
Sakata la uhamisho wa Lukaku lilichukua sura mpya msimu wa kiangazi wa 2023.
Baada ya kipindi cha mkopo Inter Milan, Lukaku alitarajiwa kurejea Chelsea, lakini pande zote mbili zilionekana kuwa na nia ya kupata suluhisho la kudumu kwingineko.
SOMA: Man Unted yawania tena saini ya Romelu Lukaku
Tetesi zilikuwa nyingi kuhusu hatima yake, huku vilabu kadhaa vikuu vya Ulaya vikionyesha nia ya kumsajili.
Juventus ilijitokeza kama mshindani mkuu, lakini mazungumzo yalikwama kutokana na tofauti za kifedha na mashabiki kupinga uhamisho huo.
Katikati ya hali ya kutokuwa na uhakika, wawakilishi wa Lukaku walichunguza fursa katika Ligi Kuu ya Saudi Arabia, ambako vilabu vilikuwa vikitoa mikataba minene.
Katika tetesi nyingine Arsenal, Atletico Madrid na Real Madrid zimeonesha nia kumsajili kiungo Adrien Rabiot ambaye anapatikana kwa uhamisho huru baada kuondoka Juventus. (Gazzetta dello Sport – Italy)
Wakala wa nyota mwingine wa Juventus, winga Federico Chiesa, yupo katika mazungumzo na Arsenal, Chelsea, Manchester United na Tottenham Hotspur. (La Stampa – Italy)
Joe Gomez anafikiria hatma yake Liverpool kufuatia kufadhaishwa na ripoti za uwezekano wa mabadilishano yanayomhusisha winga wa Newcastle United, Anthony Gordon. (Football Insider)