NCCR-Mageuzi kuboresha afya, elimu Zanzibar

ZANZIBAR: MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, Laila Rajab Khamis, amesema chama hicho kimejipanga kufanya mapinduzi makubwa katika sekta za afya na elimu endapo atapatiwa ridhaa ya kuongoza wananchi.

Akizungumza mjini Unguja katika mahojiano maalum na Daily News Digital, Laila amesema maendeleo hupatikana pale ambapo kuna kiongozi mwenye uthubutu wa kuyatekeleza. “Nipo tayari kuwatumikia wananchi wa Zanzibar na kuhakikisha huduma za afya na elimu zinaboreshwa kwa manufaa ya wote,” alisema. SOMA: NCCR Mageuzi waipa tano serikali mkataba na Dp World

Aliongeza kuwa uongozi wake utalenga pia kuboresha huduma za kijamii katika ngazi mbalimbali ili kuongeza usawa wa kijinsia. “Kwenye chama chetu ajenda ya kijinsia inazingatiwa, hususan kwa kundi la watu wenye mahitaji maalum, wanawake na vijana ambao kwa sasa wanahitaji kuangaliwa zaidi,” alisema.

Aidha, aliwaomba wananchi wote wa Zanzibar, wanawake kwa wanaume, kumpa kura katika uchaguzi mkuu ili kutimiza ndoto yake ya kuongoza kwa maendeleo endelevu. “Naombeni mjitokeze kwa wingi mnichague niwe Rais wa Zanzibar,” alisema.

Tangu mwaka 2009, Laila amekuwa mstari wa mbele katika harakati za siasa za upinzani visiwani Zanzibar na sasa amepewa imani ya kugombea urais kupitia NCCR-Mageuzi.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button