Ndalichako ataka elimu ya ufundi kuhimarishwa

WAZIRI  wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa elimu ya ufundi stadi ni vema  iimarishwe ili kutoa ujuzi kwa ajili ya kutoa nguvu kazi inayohitajika katika sekta ya ajira.

Ndalichako ameyasema hayo leo mkoani Arusha ambapo  amesisitiza  kuimarisha ujuzi unaohotajika katika soko la ajira ili kuimarishwa zaidi na  kuwajengea uwezo vijana waweze kujiajiri sanjari na kuajiri wengine ili kuinua uchumi kwa vijana wanaohitaji kuonyesha uwezo wao katika bunifu mbalimbali pamoja na miradi

Naye Dk, Adolf Rutayuga ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET)amesema kongamano hilo la siku mbili  limehudhuriwa na wadau wa ndani na nje ya nchi na ndani lengo ni kuangalia  jinsi ya kuinua ujuzi kwa vitendo unaendelezwa ili kuzalisha ajira au waweze kujiajiri.

Advertisement

Awali  Msozi Nyirenda ambaye ni Kaimu Mkurugenzi na Utafutaji Rasilimali na Mitaji amesema  suala la ajira nchini limekuwa ni changamoto kwa vijana  hivyo wameamua kutoa mafunzo ili vijana waweze kuupata utakaowasaidia kubuni mbinu mbalimbali za kibiashara ikiwemo sekta ya ajira

“Vijana zaidi ya 48000 wanefadhiliwa kwa kupewa mafunzo ili waweze kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa “

Wakati huo huo,Profesa Eddatandi  Luoga ambaye ni Kaimu Mkuu  wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)  anasisitiza mafunzo kwavitendo yanazalisha watanzania kujifunza mbinu mbalimbali katika sekta ya biashara