WAZIRI wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Deogratius Ndembeji ameipongeza sekondari ya Ntobo kwa ujenzi wa vyumba saba na matundu manane ya vyoo iliyopo katika Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Waziri Ndembeji amesema hayo leo Oktoba 6, 2024 kwenye ziara maalum ya kuangalia miradi ya maendeleo Halmashauri ya Msalala.
Waziri Ndembeji amesema serikali imetoa fedha nyingi ambapo madarasa ya kisasa yamejengwa ambapo amewataka wazazi walete watoto shuleni.
Mbunge wa Jimbo la Msalala Idd Kassimu amesema Serikali imetoa fedha nyingi imejenga maabara kwaajili ya masomo ya sayansi kufanya kwa vitendo na shilingi Milioni 600 zimejenga chuo Cha sayansi.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Ntobo Hussein Mbwambo amesema kwa asa kuna vyumba vya madarasa 22 na viti 315 na meza 315 vipo vyakutosha pia upo uwiano mzuri wa matundu ya vyoo kwa wavulana na wasichana.
Mbwambo amesema shule hiyo Ina wanafunzi 577 ambapo wasichana wanaotoka maeneo ya mbali kuna hosteli inayochukua wanafunzi 48.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha amesema madarasa yaliyojengwa ya kisasa yana feni na vigae chini.
Comments are closed.