Ndejembi kukagua miradi ya bil 71/- Iringa

IRINGA: MIRADI ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 71.46 katika sekta ya elimu ya juu na usafiri wa anga inatarajiwa kukaguliwa na Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Iringa, Oktoba 18, mwaka huu.
Miradi hiyo inahusisha uwekezaji wa Sh Bilioni 30.4 katika Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) na Sh Bilioni 41.06 katika Uwanja wa Ndege wa Iringa, uliopo kata ya Nduli, mjini Iringa.
Akizungumza na wanahabari Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema Makamu wa Rais atatembelea MUCE, ambako atakagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi saba inayolenga kuboresha miundombinu ya elimu ya juu.
Alisema miradi hiyo inajumuisha Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), wenye thamani ya Sh Bilioni 14.8, pamoja na ujenzi wa maabara ya Fizikia na hosteli ya wanafunzi unaogharimu Sh Bilioni saba.
Miradi mingine ni ujenzi wa jengo la Sayansi na jengo la Midia Anuwai na Elimu Maalum, unaogharimu Sh bilioni 7.8.
James alisema uwekezaji huo unalenga kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, kuimarisha uwezo wa chuo kutoa elimu yenye ubora na kuongeza mchango wa elimu ya juu katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Baada ya shughuli za MUCE, Makamu wa Rais anatarajiwa kuelekea Uwanja wa Ndege wa Iringa, Nduli, kukagua ujenzi wa jengo la abiria na maegesho ya magari, mradi wenye thamani ya Sh bilioni 41.06.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa, mradi huo unalenga kuboresha miundombinu na huduma za usafiri wa anga, hatua inayotarajiwa kuongeza ufanisi wa usafiri na kufungua fursa zaidi za biashara na shughuli za kiuchumi mkoani Iringa.
Amewataka wakazi wa Manispaa ya Iringa na maeneo jirani kujitokeza kushiriki katika shughuli za ziara hiyo, akieleza kuwa itakuwa fursa kwa wananchi kufahamu na kushuhudia utekelezaji wa miradi ya maendeleo mkoani humo.




Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…
THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com