Ndoa ya Wolper Novemba

MFANYABIASHARA na mbunifu wa mavazi, Rich Mitindo ambaye pia ni mzazi mwenza wa msanii wa filamu, Jaqueline Wolper ameweka wazi kuwa anatarajia kufunga pingu za maisha na nyota huyo Novemba 19, mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Rich alisema kuwa amefikia maamuzi hayo ya kufunga ndoa na Wolper baada ya kuwa naye kwenye uhusiano kwa muda mrefu hivyo anaamini umefika wakati sahihi wa kufunga ndoa.

“Sina kitu ambacho sikipendi kwa Wolper, tunaambiwa tunatakiwa kupendana bila kuangalia madhaifu yetu tumekuwa pamoja kwa kipindi kirefu na sasa umefika wakati wa kukamilisha malengo yetu ya kufunga ndoa.”

“Hii ni mipango yetu ya muda mrefu na huu ni wakati wa kuenda kutimiza kile tulichokipanga, nikisema simpendi Wolper sababu ya mapungufu yake nitakuwa ni mnafiki, nampenda kwa kila kitu ni mwanamke mpambanaji, najivunia kuwa naye amekuwa mtu muhimu kwenye maisha yangu,” alisema Mitindo.

Alisema kuwa Wolper ni mtu sahihi kwenye maisha yake na familia yake na kwa sasa wanatarajia kupata mtoto wa pili baada

Habari Zifananazo

Back to top button