Ndolezi: Kunahitajika Baraza la Vijana la Taifa

Waziri Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Vijana, Kazi na Ajira wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndolezi Petro katika mahojiano na Mwandishi wa HabariLEO, Rahimu Fadhili

DAR ES SALAAM: WAZIRI Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Vijana, Kazi na Ajira wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndolezi Petro amesema kutokuwepo kwa Baraza la Vijana Taifa, kunanyima fursa ya kuwa na Baraza la Vijana Afrika Mashariki.

Ndolezi amezungumza na HabariLEO mapema leo, ambapo amesema kuna haja ya uwepo wa Baraza la Vijana la Taifa litakalokutanisha vijana kujadili masuala ya mbalimbali ya kitaifa.

Advertisement

“Kuwa na Baraza la Vijana la Taifa ni haki ya vijana, ni sehemu ambayo watakumbushana mambo mengi, wakati mwingine wanaweza kuwa msaada wa mawazo mbadala kwa namna gani tuweze kusonga mbele,” amesema Ndolezi.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/kinana-aipa-5-act-wazalendo/

Ndolezi ameiomba serikali kuangalia kwa kina suala hilo ili kuwepo na baraza hilo litakalokutanisha vijana na kujadili masuala yao sambamba na kuibua fursa na nafasi mbalimbali.

Soma pia: https://www.instagram.com/p/CGj-Q_rlkrL/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

Februari 17, 2024 baada ya kutwaa fomu ya kugombea Uenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo alisema miongoni mwa vitu angepigania endapo angepata nafasi hiyo ni kupaza sauti juu ya upatikanaji wa Baraza la Vijana la Taifa, sambamba na kushawishi vijana wengi zaidi kujiunga na ACT Wazalendo.