Ndolezi, mgombea mwenza warejesha fomu

MHANDISI Ndolezi Petro ambaye ni mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo Taifa akimbatana na mgombea mwenza wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Malik Juma wamerudisha fomu leo.

Wawili hao wamerejesha fomu wakizindikizwa na viongozi wa Ngome ya Vijana wa mikoa ya kichama saba ya Unguja Katika ofisi za chama cha ACT-Wazalendo zilizopo Vuga Zanzibar.

Akizungumza wakati wa urejeshaji fomu hiyo, Ndolezi ametaja vipaumbele vyake kuwa ni kuiunganisha Ngome ya Vijana kuwa moja na yenye kuwasiliana kuanzia juu mpaka chini, lakini pia kuedeleza mazuri yaliyofanywa na kuboresha mapungufu yote ili kuongeza ufanisi wa ngome.

Ndolezi ameiambia HabariLEO kuwa endapo akifanikiwa kushinda nafasi hiyo ataifanya ngome hiyo kuwa jukwaa kimbilio la vijana wa Tanzania kwani atapaza sauti juu ya changamoto zao.

“Kupaza sauti juu ya upatikanaji wa Baraza la Vijana la Taifa, kushawishi vijana wengi zaidi kujiunga na ACT Wazalendo. Kufanya kazi ya kutoa elimu kwa vijana juu ya ACT Wazalendo ‘brand promise’ ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar.

” Amesema Ndolezi.

Ndolezi amesema amepanga kuimarisha mtandao wa chama mikoa yote na kuendelea kufanya kazi ya kuhamasisha usajili wa wanachama katika mfumo wa Kidigitali (ACTKiganjani).

“Kuifungua ngome kimahusiano ya kidiplomasia na vyama mbalimbali ndani na nje ya nchi sambamba na taasisi mbali mbalimbali”. Ameongeza.

Habari Zifananazo

Back to top button