Ndugai aongoza Uchaguzi wa Mwenyekiti CCM Dodoma

SPIKA wa zamani Bunge la Tanzania Job Ndugai ameibua shangwe muda mchache baada ya kukubari ombi la wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma kutaka aongoze kikao hicho.

Ndugai alijiuzulu wadhifa wake Alhamisi ya Januari 6, 2022 baada ya kumuandikia Katibu Mkuu wa CCM kuhusu nia yake ya kuachia ngazi kwa hiari, ambapo tangu afanye uamuzi huo amekuwa haonekani mara kwa mara kujihusisha na maswala ya kisiasa. Bado ni Mbunge wa Kongwa, mkoani Dodoma.

“Ninashukuru kwa heshima hii, asanteni wajumbe kwa kuniamini,” amesema Ndugai muda mfupi baada ya kuanza kuendesha kikao hicho. Kikao kilipangwa kuendeshwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa, Ndugu Godwin Mkanwa hata hivyo alijiondoa kwa kuwa anagombe nafasi hiyo kwa miaka mingine mitano.

Katika uchaguzi huo wagombea wengine wa nafasi ya Mwenyekiti ni Alhaj Adam Kimbisa na Brigedia Jenereli Agustino Gailonga.

Nafasi nyingine katika uchaguzi huo ni wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa. Pia uchaguzi huo utahusisha Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa anayewakilisha mkoa wa Dodoma.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button