Ndumbaro ataka waharifu kusemwa hadharani

KAGERA: WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amewataka wananchi kuwasema hadharani waharifu wanaofanya dhulma kwenye jamii zao.

Lakini pia hata wale wanaofanya unyanyasi unaoambatana na ukatili kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia.

Akizungumza na wananchi wa kata Nsunga wilayani Missenyi mkoani Kagera Dk Ndumbaro amesema huu ndio wakati wa kuwaweka wazi waharifu kwani kampeni hiyo haitaacha changamotoo yoyote inayohusu maswala ya kisheria.

Advertisement

“Muda wa kuwasema waharifu hadharani ni sasa, baadhi ya watu ni wanyanyasaji, wengine wamenyanganya watu ardhi ,kunyanyasa wajane, ubakaji na ulawiti, nataka kuwahakikishia wananchi kuwa kampeni  haitaacha changamotoo yoyote inayohusu sheria sisi tunasema ni haki,usawa ,na maendeleo,” amesema Ndumbaro.

Amesema kipindi cha nyuma wananchi walikuwa wakiwatafuta wanasheria na mawakili kufata huduma za kisheria lakini kwa sasa wanasheria na mawakili ndio watawafata wananchi kwenye vijiji vyao lengo la Rais Samia likiwa ni watanzania kupata haki zao.

Aidha, amesema tayari serikali imejenga jengo la mahakama katika Wilaya ya Missenyi jambo ambalo lilikuwa ni changamoto kwa miaka yote wilayani Missenyi hivyo anaamini uwepo wa jengo la mahakama umerahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi ambao walikuwa wakisafiri umbali mrefu kufata haki za mahakaman wilaya ya Bukoba.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Frankilini Rwezimula amesema  huduma za kisheria kupitia kampeni hiyo  itadumu katika Missenyi kwa siku 9 ambapo kila siku timu itasikiliza kero na changamoto za kisheria vijiji vitatu kwa siku ,ndani ya Kata kwa siku moja.

“Naomba wananchi tujitokeze kwa wingi kuleta kero zetu za kisheria ili zipate ufumbuzi ,lakini sio kero tu hata Elimu ya kisheria kujua swala lako litaenda wapi lakini pia serikali inakusaidia kupata wanasheria watakakusaidia kupata majawabu ya haki zao ,tusiwe wakimya kwa mambo yanayotuumiza,” amesema Rwezimula.

Mbunge wa Jimbo la Nkenge Frolent Kyombo amesema kuwa uwepo wa kampeni hiyo ni tunu na fursa kwa wananchi wa Missenyi kwani wananchi wengi hawana uwezo wa kujiwekea wanasheria na kuwaghamia.

Ameswma anaamini wananchi wa Missenyi kupitia kampenu hiyo watatatua changamotoo zao zinazowakabiri ,kwani baadhi ya wananchi kesi zao zimeshindwa kuendelea kutokana na kutokuwa na gharama za kuwalipa mawakili ambapo amewahakikishia wananchi wa Missenyi kuwa kampeni hiyo ya kisheria inamajawabu yao yote hivyo wasikose kujitokeza.

Ameishukuru serikali kwa kujenga jengo la mahakama katika Wilaya ya Missenyi kwani wananchi wengi wanyonge walikuwa hawana uwezo wa kusafiri kwenda mahakama ya wilaya ya Bukoba ,hivyo uwepo wa mahakama ndani ya wilaya hiyo ni sehemu ya wananchi kupata haki kutokana na chombo hicho kutoka haki kwa ka mtu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *