Nduruma wafurahia ujenzi barabara Malalua -Nduruma

ARUSHA: WANANCHI wanaoishi Kata ya Nduruma Halmashauri ya Arusha DC wameushukuru Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kujenga barabara ya Malalua -Nduruma yenye urefu wa kilomita 28 yenye thamani ya Sh bilioni 30.8.

Shukrani hizo zimetolewa na wananchi hao mara baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Asmil Ali Ussi wakati mwenge huo ulipoweka Jiwe la Msingi na kukaguliwa barabara hiyo.

Elizabeth Kaaya amesema awali barabara hiyo ya ilikuwa na changamoto sababu ya mashimo na vumbi linaloleta kero kwa wasafiri hali iliyopelekea daladala kupandisha nauli kutoka Sh 2500-3000 badala ya Sh 1500.

SOMA ZAIDI

Changamkieni mikopo asilimia 10- Kiongozi mbio za mwenge

“Sisi wananchi tunaishukuru serikali kwa kutengeneza barabara hii ya Nduruma awali ilikuwa ni kero lakini pia kwa bodaboda napo bei juu kuliko mahali unapoenda, tunaomba barabara hii ikamilike kwa wakati kwani leo wamezindua ujenzi wa mita 600,”amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button