Changamkieni mikopo asilimia 10- Kiongozi mbio za mwenge

ARUSHA: VIJANA wametakiwa kuchangamkia fursa ya mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na serikali ya asilimia 10 za mapato ya ndani ya halmashauri ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mikopo hiyo ambayo hutolewa kwa makundi ya wanawake kwa asilimia 4, vijana, asilimia 4 wanawake na na watu wenye mahitaji maalum asilimia 2 huwanufaisha wananchi hao endapo wakiitumia vizuri.

Rai hiyo imetolewa leo wilayani Arusha na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ali Ussi, alipotembelea na kukagua mradi wa uwezeshaji wananchi kiuchumi wa kikundi cha vijana cha KIVIWAMA wanaojishughulisha na ufugaji wa kuku wa mayai, katika Kata ya Malula, Halmashauri ya Meru .

Amesisitiza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais, Samia Suluhu Hassan imedhamiri kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kujiunga kwenye vikundi na kupatiwa mikopo isiyokuwa na riba ili kukabiliana na soko la ajira nchini lakini zaidi kujikwamua kiuchumi na kuwapongeza vijana wa kikundi hicho kwa kutumia vema fursa hiyo, fursa iliyowawezesha kujiajiri na kuajiri wengine.

“Niwasihi vijana wenzangu kuendelea kusimamia mradi wenu vizuri, mradi ambao unawajengea heshima kubwa kwa jamii na Taifa lenu, lakini niwasihi mkawe wajumbe kwa vijana wenzenu, wasikae vijiweni na kulalamika badala yake kutumia futsa hiyo ya mikopo waweze kujiajiri,” amesema.

Awali, Kikundi cha ufugaji wa kuku wa mayai cha KIVIWAMA chenye wanachama watano, kimepewa mkopo wa sh,milioni 25 na kukukuza mtaji wao hadi kufikia mtaji wa  Sh milioni 45.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button