Necta wapanda miti kampeni upandaji miti

BARAZA la Mtihani Tanzania NECTA limepanda miti ,zaidi ya 2000 katika shule tano za msingi katika Jiji la Tanga ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kupanda miti 100,000 kwa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu kote nchini .

Kampeni hiyo ambayo imezinduliwa na Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk Said Mohamed leo katika shule ya msingi Mleni Tanga ambapo ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

Advertisement

Amesema kuwa kampeni hiyo ambayo waliianzisha wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya NECTA inatarajiwa kufikia shule 20,000 za msingi,6000 za sekondari na vyuo vya ualimu nchini.

“NECTA imekuwa ni matumiaji mkubwa wa karatasi hivyo kutokana na umuhimu huo ndio maana tumeanza kampeni hii ya kupanda miti Kwa lengo la kuboresha mazingira yetu lakini na kuunga mkono jitihada za serikali”amesema Katibu Mtendaji huyo.