Chalamila azungumzia ulinzi AFCON 2026

DAR ES SALAAM: MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wawekezaji na taasisi mbalimbali nchini kutumia huduma za kampuni za ulinzi zilizosajiliwa ili kurahisisha ufuatiliaji wa matukio ya kiusalama yanapotokea.

Chalamila amesema hayo leo Mei 25, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo kuhusu maandalizi ya ulinzi na usalama kuelekea mashindano ya AFCON 2027.

Akizungumzia tukio la kuuawa kwa raia wa China anayodaiwa kuuawa na watu wanaosadikika kuwa walinzi wa kiwanda kufuatia tuhuma za kutoroka na Sh milioni 10, Chalamila amesema matumizi ya walinzi walio nje ya mfumo rasmi wa kampuni za ulinzi yanaweza kuikwamisha serikali kuwabaini wahusika kwa haraka.

Amesisitiza kuwa uwepo wa kampuni rasmi za ulinzi husaidia mamlaka kufanya uchunguzi kwa urahisi na kuongeza uwajibikaji pale matukio ya uhalifu yanapotokea.

Aidha, ametoa wito kwa wawekezaji na taasisi kuhakikisha wanazingatia taratibu za usalama kwa kushirikiana na kampuni zinazotambulika kisheria ili kulinda watu na mali zao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button