NEMC yajipanga mashindano ya SHIMMUTA 2025

DAR ES SALAAM: Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limejipanga kushiriki mashindano ya michezo yanayoratibiwa na Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, taasisi na kampuni binafsi Tanzania (SHIMMUTA) ambapo leo Oktoba 28, 2025 limezindua rasmi vifaa vilivyofadhiliwa na Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (Adaptation fund) vitakavyotumika na wanamichezo katika mashindano hayo.
Akizungumza wakati kukabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dk Immaculate Sware Semesi amesema michezo ni muhimu kwa afya ya binadamu kwani hupelekea uwezo wa kufanya kazi vizuri huku akisisitiza usimamizi na uhifadhi wa mazingira nchini.

Ameongeza kuwa ushiriki wa NEMC katika michezo hiyo ni fursa muhimu ya kuifikia jamii, kuimarisha ushirikiano baina ya watumishi wa umma na sekta binafsi.
Mwenyekiti wa Michezo, NEMC Fortinatus Patrick amesema timu za NEMC ziko tayari kwenda kupambana katika michezo yote na wamejiandaa kufanya vizuri katika mashindano ya mwaka huu.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Fedha (NEMC) Dickson Mjinja ambaye ni mlezi qa timu hiyo, alipozungumza amesema NEMC imejipanga kisawasawa kuwa washindani na si washiriki katika michezo yote iliyo jisajili.
NEMC kwa kushirikiana na Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi umefanikisha mandalizi hayo ya SHIMMUTA 2025 yanayotarajiwa kuafanyika jijini Mwanza November 13 – 29, 2025 huku ikilenga kuelimisha umma wa watanzania kuhusu mazingira na masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi.





Begin now earning every month an extra amount of $17k or more just by doing very simple and easy online job from home. I have received $18953 in my last month direct in my bank acc by doing this easy home base job just in my part time for 2 hrs maximum a day online. Even a child can now do this job and earns money online. Everybody can get this home job right now and start earning dollars online by follow details here……….
Click the link—↠ https://www.Homeprofit1.site
I’m making over $25,000 a month working part-time. I kept hearing other people talk about how much money they were making online, so I decided to look into it. Well, it’s all true and has completely changed my life. This is what I do. Check it out by visiting the following link:
COPY THIS →→→→ http://Www.Work99.Site