Ngoma aibeba Simba mabegani

ZANZIBAR : KATIKA anga la mpira wa miguu wa Afrika, Jumapili hii ya Mei 25, macho na masikio yatakuwa visiwani Zanzibar, Uwanja wa New Amaan Complex,  wakati Simba itataka  kupindua kupindua matokeo kwa kutafuta ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya RS Berkane na kujihakikishia taji la Kombe la Shirikisho Afrika.
Lakini kwenye sakata hili la kusisimua, jina moja linang’ara kama taa ya matumaini kwa Wekundu wa Msimbazi Fabrice Ngoma.

Kiungo huyo mwenye uzoefu mkubwa katika fainali za kimataifa, sasa amegeuka kuwa mhimili wa matumaini na kiongozi wa wachezaji wachanga ndani ya kikosi cha Simba.

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids, hakusita kuweka wazi umuhimu wa Ngoma katika mchezo huu wa marudiano.

“Wengi wa wachezaji wetu ni wachanga, hawajawahi kuwa kwenye mazingira kama haya isipokuwa Ngoma. Ana uzoefu, utulivu, na uongozi unaohitajika kuwavuta wengine juu,” amesema Fadlu.

Kwa upande wake, Ngoma anaonekana kuwa katika hali ya utayari wa juu, si tu kwa sababu ya uwezo wake wa kiufundi, bali kwa mzigo mkubwa wa matumaini aliopewa. Amebeba Simba mabegani  kwa kuongoza kwa ari, kuwatia moyo vijana wenzake, na kuhimiza umoja ndani ya kikosi.

Simba inatakiwa kushinda kwa tofauti ya mabao matatu ili kunyakuwa taji, baada ya kupoteza kwa 2-0 katika mchezo wa kwanza. Uwanja nao umekuwa gumzo, Benjamin Mkapa si mahala pa vita tena, badala yake mapambano yatafanyika Zanzibar.

Lakini kwa mtazamo wa Fadlu, uwanja wa nyumbani una tafsiri pana zaidi. “Hapa Zanzibar, bado tuko nyumbani, tunaamini fahari ya watu wa Zanzibar itakuwa nyuma yetu – na hilo linaweza kuleta tofauti kubwa kiakili na kisaikolojia.”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button