Ni vita ‘dabi’ nusu fainali Ngao ya Jamii leo

Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es Salaam utakaotumika kwa mchezo wa nusu fainali ya pili ya Ngao ya Jamii leo.

NUSU fainali ya kibabe ya mchezo wa ‘dabi’ Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba inapigwa leo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Michuano ya Ngao ya Jamii huashiria ufunguzi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo imepangwa kuanza Agosti 16.

SOMA: Yanga vs Simba Ngao ya Jamii Agosti 8

Advertisement

Yanga na Simba zilikutana kwa mara ya mwisho Aprili 20 katika mchezo ya Ligi Kuu msimu wa 2023/2024 Yanga ikishinda kwa mabao 2-1.

Mchezo huo utakuwa nusu fainali ya pili baada ya Azam na Coastal Union kupepetana katika nusu fainali ya kwanza kwenye uwanja wa New Aman, Zanzibar.

Azam na Coastal Union zilitoka sare ya bao 1-1 zilipokutana kwa mara ya mwisho katika mchezo wa Ligi Kuu Machi 6, 2024.