Venezuela: Rais Nicolás Maduro ameshinda uchaguzi wa urais wa Venezuela, kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyotolewa na Baraza la Uchaguzi. Nchini humo.
Mkuu wa Baraza la Kitaifa(CNE) Elvis Amoroso amesema kwamba asilimia 80 ya kura zilizohesabiwa Nicholas Maduro amepata asilimia 51.2, huku mpinzani wake, Edmundo González, akipata asilimia 44.2.
Kambi ya Upinzani nchini humo inadai kuwa mchakato wa kuhesabu kura ulijaa udanganyifu, na wameapa kupinga matokeo hayo.
Akizungumza na wananchi mjini Caracas, Rais Maduro amesema ushindi wake ni alama ya amani na utulivu.
“uchaguzi huu umefanyika kwa uwazi nashangaa kuona wapinzani wakilia na udanganyifu wa kura kila siku”, amesema Maduro.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken, ameonesha kutoridhika na matokeo hayo, akisema matokeo hayo hayakuwakilisha kura za watu wa Venezuela.
Tangu mwanzo wa mchakato wa uchaguzi, kambi ya upinzani imekuwa ikitumia maelfu ya waangalizi katika vituo vya kupigia kura ili kuhakikisha ulinzi wa kura zao unalindwa.
Rais Nicholas Maduro ameshika wadhifa wa urais wa Venezuela kwa kipindi cha miaka 11 tangu alipoingia madarakani.

SOMA: Tanzania, Venezuela zakubaliana kushirikiana kisiasa