Nicolas Maduro kuapishwa tena kwa muhula wa tatu

VENEZUELA : RAIS Nicolas Maduro wa Venezuela anaapishwa leo kwa muhula wake wa tatu wa miaka sita, kufuatia uchaguzi wa Julai 2024 uliojaa tuhuma za udanganyifu.
Kuapishwa kwake kumegubikwa na maandamano ya upinzani na kutekwa kwa kiongozi wa upinzani Maria Corina Machado, ambaye alizuiwa kushiriki uchaguzi.
Vyama vya upinzani vimeandamana kote nchini kumshinikiza Maduro, huku Marekani ikitaja vitendo vya utawala wake dhidi ya wapinzani kuwa vya kiunyanyasaji.
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amemtetea upinzani wa Venezuela, akisema hawapaswi kudhuriwa kwa kushiriki maandamano. SOMA: Uteuzi wa Rais Maduro hali ni tete