Niger: Jenerali.Tchiani aongezewa miaka mitano

NIGER : MKUU wa jeshi la Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani, ameapishwa kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.
Tchiani ameiongoza Niger tangu 2023 baada ya kumuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum kupitia mapinduzi ya kijeshi.
Chini ya katiba mpya, Jenerali Tchiani amepandishwa cheo hadi jenerali wa juu wa jeshi na kutangaza kuvunjwa kwa vyama vyote vya kisiasa.
Akizungumza katika hafla ya kuapishwa mjini Niamey, aliahidi kuwatumikia wananchi kwa uaminifu. SOMA: NIGERIA: Hatma ya Burkina Faso, Mali na Niger kujulikana kesho
Niger imekumbwa na mashambulizi ya wanajihadi kwa miaka mingi, hali iliyochangia mapinduzi hayo. Nchi hiyo, pamoja na Mali, Guinea na Burkina Faso, imekata uhusiano na Ufaransa na kuimarisha ushirikiano na Urusi.
Aidha, Niger na nchi hizo, isipokuwa Guinea, zimejiondoa Ecowas, huku mvutano na jumuiya hiyo ukianza baada ya junta kupendekeza mpito wa miaka mitatu kuelekea utawala wa kidemokrasia.



