Njaa yauwa Kaskazini Ethiopia

MTU mmoja kati ya watatu Kaskazini mwa Ethiopia wanakabiliwa na njaa kali, shirika la misaada lenye makao yake makuu nchini Uingereza Oxfam linasema.

Hiyo ni jumla ya watu milioni 10 katika mikoa ya Tigray na Amhara.

Migogoro na ukame vimepunguza kwa kiasi kikubwa mavuno na kulazimisha mamilioni ya watu kukimbilia kile ambacho shirika la misaada linaita “njia zisizofikirika za kuishi.”

Advertisement

Ripoti ya wakala wa serikali ya shirikisho ilisema karibu watu 400 tayari wamekufa katika mikoa hiyo kutokana na njaa.

Lakini hili lilipingwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, ambaye alisema hakuna vifo vilivyotokea nchini humo kwa sababu ya njaa pekee.

Isipokuwa juhudi za usaidizi hazijaongezwa, Oxfam inaonya kwamba Kaskazini mwa Ethiopia kunaweza kuona janga la kibinadamu linalozidi kuwa mbaya.