Njaa yazidisha utapiamlo Afrika

LONDON: SHIRIKA la kimataifa la hisani kwa watoto, Save the Children, limesema kuwa takribani nchi nne za Afrika zinatarajiwa kukumbwa na upungufu wa chakula maalum cha kuokoa maisha ya watoto waliokumbwa na utapiamlo katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

Mkurugenzi wa shirika hilo Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Yvonne Arunga, alisema kuwa wakati njaa ikizidi kuutikisa ulimwengu, ufadhili ambao ungeweza kuokoa maisha ya watoto umepungua kutokana na kukatwa kwa misaada katika siku za karibuni.

Kwa mujibu wa Save the Children, ugavi wa vyakula maalum vyenye virutubisho na madini pamoja na huduma nyingine za kimatibabu umepungua zaidi katika nchi za Nigeria, Kenya, Somalia na Sudan Kusini. SOMA: Wanafunzi Handeni, Mkinga kupewa chakula bure shuleni 

Imeelezwa kuwa baadhi ya zahanati kwenye nchi hizo zimeanza kutumia huduma za matibabu ambazo si rafiki kwa afya ya watoto wenye utapiamlo, hali inayoongeza hatari kwa maisha ya watoto wengi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button