Nkoronko atangaza nia ubunge Sumbawanga

SUMBAWANGA:MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mbonimpaye Ntiyonza Nkoronko ametangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge wa Sumbawanga Mjini kupitia chama hicho.
Akizungumza na mtandao huu mapema leo, Nkoronko amesema amefikia hatua hiyo baada ya kutambua hatma ya dunia ipo mikononi mwa vijana.

“Vijana wenzangu hatutakiwi kuogopa kuonyesha uwezo wetu, tu a nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko katika jamii,” amesema.
Jimbo la Sumbawanga Mjini lina kata 19, ambalo liko Mkoa wa Rukwa.

