NMB yatoa vifaa vya afya, elimu Kagera

KAGERA: Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya elimu na Afya vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 103.2 kwa shule za msingi, sekondari na zahanati mkoani Kagera.

Hatua hiyo ni sehemu ya kurejesha kwa jamii na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.

Msaada huo umepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima katika hafla iliyofanyika Shule ya Msingi Mgeza Mseto.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na viti mwendo huku Halmashauri za Bukoba,Manispaa ya Bukoba, Muleba na Missenyi nao wakinufaika na msaada huo.

Akiwasilisha taarifa kwa niaba ya NMB, Meneja wa Kanda ya Ziwa, Faraja Ng’ingo amesema benki hiyo inaendelea kujikita katika kusaidia jamii, akibainisha kuwa hadi sasa NMB ina wateja zaidi ya milioni 8, huku tangu mwaka 2021 ikiwa imerejesha kwa jamii zaidi ya Sh Bilioni 24 katika miradi mbalimbali bara na visiwani.

Amesema msaada huo unalenga kupunguza changamoto za vifaa mashuleni na kuboresha huduma za afya katika zahanati.

Vifaaa vilivyotolea ni viti Mwendo,Madawati ,vitanda vya mabweni ,mashuka,vifaaa vya kuezeka zahanati samani mbalimbali kwa Magereza.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima, aliyekuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, amesema vifaa hivyo vitatumika kama ilivyokusudiwa na vitasaidia kupunguza changamoto za wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo kutokana na uhaba wa vifaa.

Aidha, amewahimiza wadau na wananchi wengine kuiga mfano huo kwa kuwajali watoto wenye mahitaji maalumu hata katika matukio binafsi kama sherehe za kuzaliwa.

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa ya Bukoba, Mheshimiwa Acton Rwankomezi, ameishukuru NMB kwa mchango huo, akieleza kuwa bado manispaa inakabiliwa na upungufu wa zaidi ya madawati 1,000. Amesema msaada uliotolewa, ukiwemo wa madawati, utasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto hiyo.

Nao walimu pamoja na walezi wa watoto wenye mahitaji maalumu wamepongeza msaada huo na kuitaka jamii kuendelea kushirikiana kusaidia kundi hilo muhimu.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.FindJobs1.Site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button