NSSF yafikia Sh tril 8.5/-

DAR ES SALAAM: Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeongezeka kutoka S tirioni 4.8 mwaka 2021 hadi kufikia tirioni 8.5 mwaka 2024 ongezeko hilo likichangiwa kutokana na wingi wa waajiri na waajiriwa.

Hayo ameyasema leo Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii (NSSF)Masha Mshomba kwenye mkutano na jukwaa la wahariri Tanzania (TEF)

Mshomba amesema maboresho ya mfumo wa tehema pia imechangia kuongezeka kwa fedha hizo kwenye mfuko wa hifadhi wa jamii ambapo mpaka kufikia mwaka 2025 wanatarajia kufika asilimia 82 kwenye Tehama ya mfuko huo.

Aidha Mshomba amesema maboresho hayo ya mfumo wa Tehama imesaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa usumbufu wa wateja kwenda ofisini kwani wanaweza kufanya kidijitali ambapo inaendana na kasi ya mabadiliko ya Dunia kwenye Tehama.

Aidha amesema serikali inatoa mchango mkubwa kwenye mfuko huo wa hifadhi ya jamii na wao kama mfuko wanaweka mazingira mazuri ya watumishi,uadilifu pamoja na Tehama.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa uwezeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Omary Mziya amesema wameanzisha skimu ya Taifa ya hifadhi ya jamii sekta isiyo rasmi yaani (National Informal Sector Scheme -NISS) iliyoanzishwa mwaka 2018 yenye lengo la kuongeza wigo kwenye hifadhi ya jamii na makundi yasiyonufaika na huduma hizo pamoja na kuchochea maendeleo na kasi ya kiuchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Nae Meneja wa mifumo kutoka Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) Mihayo Selemani amesema lengo la matumizi ya tehama kwenye mfuko wa hifadhi hiyo ni kuhakikisha wanachama wote wanapata huduma zote katika lango la huduma kwenye mfuko huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri (TEF)Deudatus Balile amesema ameshukuru mfuko huo wa semina hiyo kwa wahariri huku akishauri kuwa mfuko huo uwekezekeze kwenye miradi ya kimkakati pamoja na ajenda ya msingi ya uwekezaji kwa maendeleo ya nchi.

Habari Zifananazo

Back to top button