Nyakafulu yapata bil 3/- za maendeleo

GEITA: KATA ya Nyakafulu iliyopo Wilaya ya Mbongwe Mkoa wa Geita imepokea Sh bilioni 3 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ndani ya miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan madarakani.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella amesema hayo alipozungumza na wachimbaji wadogo wa mgodi wa Isanjabadugu uliopo katika kata hiyo.

Shigella amewapongeza wachimbaji hao na kuwataka kuendelea kujituma na kuchangia katika pato la halmashauri na taifa kwa ujumla.

SOMA: Wachimbaji wadogo mambo safi sekta ya madini

Aidha, mbali na kuongea na wachimbaji wadogo, Shigella pia amefanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotarajiwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru wilayani hapo.

Miradi iliyokaguliwa ni wa kituo cha afya Lugunga ambao umejengwa kwa fedha za Tasaf na  unatarajiwa kuwekewa jiwe la msingi  pamoja na Shule ya Sekondari Bugegere inayotarajiwa kuzinduliwa.

SOMA: Serikali kupiga jeki wachimbaji wadogo

Wakati huo huo, Shigella amewasihi  wananchi wa Geita kuwekeza kwenye elimu kwa kuhakikisha watoto wanaenda shule kutokana na kipato wanachokipata kwa kazi ya mikono yao.

Habari Zifananazo

Back to top button