Nyie Simba hiyo namba 6 mtaua watu kwa presha!

DARES SALAAM; MUDA mfupi baada ya usiku huu klabu ya Yanga Yanga ya Dar es Salaam kutambulisha usajili mpya wa kiungo wa boli kutoka Stade Malien ya Mali, Lassine Kouma, watani wao Simba nao dakika chache baadaye kwenye mitandao ya kijamii wameweka jezi yenye namba 6 na kuzua gumzo mtandaoni kwa wadau wa soka kila mmoja akitafsiri anavyoelewa.
‘Code’ imezidi kuwa ngumu hasa baada ya kuonekana aliyeposti amefanya hivyo akiwa Zanzibar. Je namba 6 ina maana gani? Ni yule anayehusishwa akitokea Zanzibar? Au Simba wanashusha kifaa gani?



