MANCHESTER United itawakosa wachezaji 13 katika mchezo wa EPL dhidi ya Liverpool Jumapili hii.
Wachezaji hao ni Marcus Rashford na Anthony Martial ambao wote wanaumwa, Victor Linderof anasumbuliwa na goti, Harry Maguire ana maumivu ya kinena.
Luke Shaw anasumbuliwa na misuli ya paja, Casemiro ana maumivu ya paja, Jadon Sancho sababu za kinidhamu.
Wengine ni Lisandro Martinez anasumbuliwa na kifundo cha mguu, Tyrell Malacia, Christian Eriksen goti, Amad Diallo na Mason Mount wote wana maumivu ya goti.
Nahodha Bruno Fernandez pia atakosekana kutokana na adhabu ya kadi tano za njano.
Bruno alioneshwa kadi ya tano ya njano katika mchezo dhidi ya Bournemouth waliopoteza mabao 3-0 uwanja wa Old Trafford.