Nyuki wa Tabora washindwa kung’ata

KLABU ya Fountain Gate imezima matumaini ya wenyeji Tabora United ya kunyakua pointi 3 muhimu baada ya kuwachapa nyuki hao wa Tabora mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.