Ofisi ya msajili wa hazina yaandaa CEO Forum 2025

DAR-ES-SA;AAM : OFISI ya Msajili wa Hazina imeandaa kikao kazi maalum ‘CEO Forum 2025’ kitakachowaleta pamoja Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa mashirika ya umma nchini wapatao 700.

Hayo yamesemwa Leo Agost 11 Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utendaji, Ufuatiliaji na Tathmini Mashirika ya Umma ya kibiashara, Lightness Mauki amesema mkutano huo unalenga kujadili kwa kina jinsi taasisi za umma zinavyoweza kuwa shindani katika soko la kimataifa, kuongeza mapato yasiyo ya kodi, na kushiriki kikamilifu katika kuendesha uchumi wa kisasa unaoongozwa na matokeo.

Amesema Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Agosti 23-26 jijini Arusha, utapitia mijadala ya kitaasisi, Serikali inalenga kuimarisha ufanisi, uwajibikaji na ubunifu katika taasisi hizi ili ziweze kuwa wabia halisi wa maendeleo ya Taifa. SOMA: Mashirika ya umma yamilikia ardhi bila hatimiliki

Lightness amesema  kipaumbele kitawekwa katika kufanikisha utekelezaji wa Dira 2050, kwa kuhakikisha taasisi za umma zinajipanga kuwa wabia wa kweli wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kwa mujibu wa Dira 2050, Serikali imedhamiria kuwa na uchumi wa kati wa juu ifikapo mwaka 2050, huku pato la Taifa likifikia $1 trilioni na pato la mtu mmoja mmoja $7000 kwa mwaka.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button