PAC yataka ziwekwe samani ATC kampasi ya Kikuletwa

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imekiagiza Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kuweka samani katika majengo mbalimbali yaliyopo kampasi ya Kikuletwa ikiwemo ujenzi wa mtambo wa kituo cha kufua umeme unaotumia nguvu za maji kwa nia ya kufanya tafiti za umeme kwa wanafunzi wanasoma eneo hilo.

Pongezi hizo zimetolewa  wilayani Hai mkoani Kilimanjaro  na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Japhet Hasunga pamoja na wajumbe wa kamati hiyo wakati walipotembelea eneo hilo na kujionea uhalisia wa ujenzi wa kituo cha kufua umeme sanjari na majengo mbalimbali yaliyojengwa na serikali kupitia Mradi wa Ushirikiano wa Kikanda wa Afrika Mashariku(EASTRIP).

Hasunga amepongeza juhudi za serikali katika kuhakikisha kampasi hiyo inakuwa mahiri katika ufundishaji wanafunzi kwa vitendo na kuagiza samani pamoja na mahitaji mengine muhimu yawepo ili wa mafunzo hao w watakapoanza masomo kwenye kampasi hiyo wasikumbane na changamoto za vifaa vya kujifunzia ikiwemo samani

“ATC mnahitaji pongezi kwanza  ni kwa mradi huu wa umeme lakini pia majengo yenu ni ya kisasa hapa Rais Samia Suluhu Hassan  ametekeleza sera ya elimu kwa vitendo zaidi, thamani ya fedha inaonekana”

Naye Mhandisi mshauri wa mradi huo, Robert Kabudi  amesema mradi huo ulianza Mei 13,2024 na unatarajia kukamilika Oktoba 13 ,2025 na kwa sasa mradi huo unaendelea huku wakisubiri mitambo inayotengenezwa nje ya nchi ifike nchini lakini ukikamilka utasaidia vijiji vya jirani ikiwemo kutumika kama kiwanda cha kufundishia wanafunzi kwa vitendo jinsi ya kuzalisha umeme na kinatarajia kutoa megawati 1.65 .

Amesema mradi huo wa mtambo wa kufua umeme unafanyika kwa awamu tatu na kwa sasa upo katika utekelezaji wa awamu ya kwanza na umefikia asilimia 20  wenye thamani ya zaidi ya Sh  bilioni 9.930 ambao ukikamilka utasaidia wanafunzi wanaosoma kampasi hiyo kufanya kazi kwa vitendo.

Wakati huo huo, Mkuu wa Chuo cha ATC, Profesa Musa Chacha amesema  chuo hicho kilipokea kiasi cha sh, bilioni 37.657 kwaajili ya ujenzi wa majengo 11 katika kampasi ya Kikuletwa ikiwemo hosteli, bwalo la chakula na nyumba za maunganisho ya umeme, jengo moja lenye madarasa matano ikiwemo ukumbi wa mihadhara na karakana tatu

Huku baadhi ya wabunge wa kamati hiyo, Esther Matiko mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mara na Emmanuel ole Shangai kutoka Jimbo la Ngorongoro wamepongeza serikali kwa kutoa fedha kwaajili ya chuo hicho ikiwemo uzalishaji wa umeme wenye tija zaidi kwa nchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button