Papa hali tete

ROMA: VATICAN imetangaza kuwa Papa Francis bado yuko katika hali tete, huku vipimo vya damu vikionyesha dalili za awali za figo zake kufeli.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki mwenye umri wa miaka ,88, anapambana na matatizo ya afya ambayo yameathiri mfumo wake wa upumuaji na figo.
Hata hivyo, hali yake imeendelea kudhibitiwa na wataalamu wa afya kwa kiwango cha juu, na ameendelea kupambana na nimonia inayoshambulia mapafu yake yote mawili. Hali hii imesababisha kulazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki moja.
Soma zaidi: Papa Francis alazwa
Kwa mujibu wa ripoti ya CNN, Papa Francis hajaonyesha matatizo yoyote makubwa ya kupumua tangu jana jioni, na hali yake inaonekana kuwa imedhibitiwa kwa sasa.
Taarifa kutoka Vatican zinaeleza kuwa vipimo vya damu vinaonyesha dalili za awali za kushindwa kwa figo zake, lakini hali hiyo inaendelea kufuatiliwa kwa karibu.
Soma zaidi: Papa Francis, asumbuliwa homa ya mapafu
Viongozi wa imani na waumini kutoka duniani kote wameungana katika maombi kwa ajili ya afya ya Papa Francis. Aidha, ratiba yake imepangwa upya kutokana na matibabu anayopokea hospitalini.
Papa Francis, ambaye ni kiongozi wa kiroho wa Kanisa Katoliki, amekuwa akiongoza kanisa hilo kwa miaka mingi, na jamii ya waumini inajiandaa kumwombea kwa ajili ya kupona kwake.



