FAINALI ya mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga Princess na JKT Tanzania inapigwa leo Dar es Salaam.
Mechi hiyo ya fainali kwenye uwanja wa KMC itatanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Simba Queens na Ceasiaa Queens.
SOMA: JKT Queens yafanya mauaji Ngao ya Jamii
Yanga Princess iliitoa Simba Queens katika nusu fainali kwa mikwaju ya penalti 4-3 wakati JKT Queens ilitinga fainali kushusha kipigo kizito dhidi ya Ceasiaa Queens cha mabao 7-0.
Simba Queens ilikuwa mtetezi wa taji hilo.
Kufanyika kwa mechi za Ngao ya Jamii wanawake ni kiashiria kuelekea kuanza kwa Ligi Kuu ya wanawake Tanzania Bara msimu wa 2024/2025.