Pauni mil 33 kumpeleka Khusanov Man City
KLABU ya Manchester City imekubaliana dili la pauni milioni 33.6 na Lens ya Ufaransa kwa ajili ya kumsajili beki wa kati Abdukodir Khusanov. (BBC)
Aidha tetesi za usajili zinaonesha kuwa Aston Villa imeongeza dau lake kwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Donyell Malen hadi pauni milioni 21, lakini klabu hiyo ya Ujerumani bado inataka ilipwe pauni milioni 25.1 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25. (Florian Plettenberg)
Manchester United, Arsenal na Liverpool zinavutiwa na kiungo wa Wolves raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 23, Joao Gomes. (Sun)
Monaco ni klabu ya hivi karibuni kuonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United mwenye umri wa miaka 27, Marcus Rashford. (Telegraph)
Paris Saint-Germain inavutiwa na mshambuliaji wa Aston Villa raia wa Colombia mwenye umri wa miaka 21, Jhon Duran. (RMC Sport)
Manchester United inafanya kila linalowezekana kuishinda Tottenham Hotspur kumsajili mshambuliaji wa Paris Saint-Germain raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26, Randal Kolo Muani. (Teamtalk)



