

Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akibariki na kuzindua hospitali ya saratani-Good Samaritan iliyopo Jimbo Katoliki Ifakara leo.
Uzinduzi huo umehudhuria na wageni mbalimbali wakiwemo Maaskofu, Wakuu wa Mashirika ya Kimisionari na Kitawa, mapadre kutoka ndani na nje ya Jimbo Katoliki Ifakara, watawa wa kiume na Kike na baadhi ya waumini wa Jimbo hilo.