Polisi kuimarisha ulinzi Kusini Unguja siku ya Eid El-Fitr

JESHI la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja limeahidi kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mkoa huo wakati wa Sikukuu ya Eid El-Fitr ili kuhakikisha wananchi wanasherehekea kwa amani na usalama.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya Polisi Mkoa huo, Tunguu, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Daniel Shillah amesema kuwa jeshi la polisi litachukua hatua madhubuti kubaini, kudhibiti na kutanzua matukio yote ya kihalifu katika kipindi hicho cha sikukuu.

Aidha, Kamanda Shillah ametoa onyo kwa madereva dhidi ya uvunjaji wa sheria za usalama barabarani hasa wanapowabeba abiria kuelekea viwanja na kumbi za starehe.

Vilevile, amewataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa za viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani ili kusaidia kudumisha usalama katika mkoa huo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button