MKUU wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mrakibu wa Polisi (SP) Solomon Mwangamilo, kwa kushirikiana na viongozi wa waendesha pikipiki (bodaboda), wamewatembelea wagonjwa wa ajali za bodaboda na vyombo vingine vya moto Hospitali ya Nkoranga Lutheran Hospital iliyopo Arumeru Mkoani Arusha.
Akiongozana na askari wakikosi hicho, mkuu huyo amesema lengo la kufika katika hospitali hiyo ni kukusanya taarifa zao na kutoa pole kwao, ambapo amebainisha kuwa hospitali hiyo ni maarufu kwa kutibu magonjwa waliopata madhara yatokanayo na ajali mbalimbali.
Naye Katibu wa waendesha bodaboda Wilaya ya Arusha, Hakimu Msemo, amebainisha kuwa wapo baadhi ya waendesha pikipiki, ambao wamekuwa wakiendesha vyombo hivyo kwa kukiuka sheria za usalama barabarani na kueleza kuwa kutokana na ziara hiyo, watakuwa mabalozi wazuri kwa wenzao.