Pombe chupa mbili kwa mwanaume, moja mwanamke

MWANAUME anatakiwa kunywa uniti mbili za bia sawa na chupa mbili wakati mwanamke anapawa kunywa unit moja ambayo ni sawa na chupa moja ili kuepuka magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo Moyo.

Hayo yamesemwa leo Septemba 29, 2022 na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Tatizo Waane ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Moyo Duniani.

Dokta Waane amesema unywaji pombe kupita kiasi ni miongoni mwa sababu kubwa inayosababisha magonjwa ya moyo.

Sababu zingine zilizotajiwa ni mtindo mbaya  wa maisha ikiwemo ulaji na kutokufanya mazoezi.

Amesema Pombe inafanya misuli ya moyo kulainika na inapolainika inakosa  nguvu na moyo unashindwa kufanya kazi kama inavyotakiwa.

“Lakini unapokuwa na matumizi ya pombe  kupita kiasi inachangia tabia nyingine kama mtindo wa maisha utakuwa unakula na ndizi ,nyama choma,tumbaku sigara kwa hiyo vitu hiyo ni hatari,’amesisitiza.

|Aidha, amewashauri kwa wale ambao hawanyi pombe wasinywe na kwa wale ambao wanatumia wapunguze matumizi au kuacha kabisa.

Dk Waane ambaye pia ni Mkurugenzi wa tiba JKCI amesema wagonjwa wamoyo wanaongezeka ambapo awali walikuwa wanapoke wagonjwa 50 hadi 60 kwa siku na hivi karibuni wagonjwa wamefika 300 hadi 500 kwa siku.

Habari Zifananazo

Back to top button