PPRA yataka usajili watu 100,000 kufikia Disemba

MTWARA: MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma Nchini (PPRA) Dennis Simba
amesema lengo la mamlaka hiyo ni kuhakikisha wanasajili vikundi zaidi ya laki moja hadi kufikia Disemba 2026.

Hayo yamejiri wakati Mwenge wa Uhuru mwaka 2026 ulipowasili mkoani humo Mei 3, 2026 ukitokea mkoani Lindi na kuanza kukimbizwa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Akizungumza katika viwanja vya sabasaba ambako mkesha wa Mwenge huo wa Uhuru umefanyika katika manispaa hiyo,  mkurugenzi mkuu huyo wa PPRA amesema tangu kuanza ukimbizwaji wa mwenge ongezeko hilo la usajili wa vikundi limekuwa kwa kasi.

Amesema kabla ya mwenge wa uhuru walikuwa na vikundi 700 na mpaka sasa tayari wamesajiri zaidi ya vikundi 1,500  mwaka huu baada ya kuanza kampeni hizo.

‘’Lengo letu mpaka mwenge unaisha kufikia hata Oktoba tuwe tumesajili vikundi 20 elfu lakini huo ni mwanzo, lengo la PPRA ni kuhakikisha tunasajili vikundi zaidi ya laki moja hadi kufikia Disemba mwaka huu’’amesema Simba

Ofisa Maendeleo ya Jamii wa manispaa hiyo, Sofia Halidi amesema mwaka 2025/2026 manispaa hiyo imesajili na kuhaulisha vikundi 126 ambapo kati ya hivyo vikundi 81 vimewasilishwa kwenye mamlaka hiyo.

Hata hivyo kati ya vikundi  hivyo 81 vikundi 13 vimeshasajiliwa na kufambulika rasmi na mfumo wa ununuzi wa umma (NeST) na katika vikundi hivyo 13 ikiwemo vikundi 9 ni vijana, vikundi 3 wanawake na 1 cha watu wenye ulemavu.

‘’Usajiri bado unaendelea kupitia mamlaka husika PPRA na kati ya vikundi 13 vilivyosajiliwa vikundi 6 vimeanza kunufaika kwenye mfumo wa  ununuzi wa umma na thamani ya kazi walizofanya ni zaidi ya Sh milioni 200’’

Aidha halmashauri hiyo inaendelea kuhamasisha jamii kujiunga pamoja katika vikundi na kuwa na shughuli ya pamoja ili wawe na sifa ya kusajiliwa kwenya mfumo huo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button